UTUME WA KANISA
TAMKO LA UTUME LA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO
Utume Wetu
Kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, wanaoishi kama mashahidi Wake wa upendo na kutangaza kwa watu wote injili ya milele ya Ujumbe wa Malaika Watatu, kwa ajili ya maandalizi ya kurudi Kwake hivi karibuni (Mathayo 28:18-20, Matendo 1:8, Ufunuo 14:6-12).
Njia Yetu ya Utekelezaji
Tukiongozwa na Biblia na Roho Mtakatifu, Waadventista wa Sabato hutekeleza utume wa kuwafanya watu kuwa wanafunzi kupitia maisha ya mfano wa Kristo, uponyaji, huduma, kutangaza, kufundisha, na kutoa mafunzo ya vitendo.
Maono/Njozi Yetu
Kwa kupatana na ufunuo wa Biblia, Waadventista wa Sabato huona kilele cha mpango wa Mungu wa urejeshwaji wa viumbe vyake vyote katika umoja kamili na mapenzi yake makamilifu na haki Yake.